Quantcast
Channel: Global Voices in Swahili » Kenya
Viewing all 29 articles
Browse latest View live

Mwaliko wa Mapendekezo ya Tuzo za Blogu Nchini Kenya 2014

$
0
0

Waandaaji wa Tuzo za Blogu nchini Kenya 2014, ambao ni Umoja wa Wanablogu nchini humo (BAKE) kwa sasa wanakaribisha mapendekezo ya wawaniaji wa tuzo hizo mpaka Februari 10, 2014.  Watumiaji wanaweza kupiga kura kwa njia ya mtandao kuanzia Machi 1, mpaka April 30, 2014 kupendekeza blogu wanazoona kuwa ni bora katika makundi 17 tofauti, ikiwa ni pamoja na kundi jipya la Blogu bora ya Afya na Blogu Bora ya Kaunti/Wilaya.

Bake logo

Nembo rasmi ya BAKE. Picha imetolewa: http://bloggers.or.ke.

Tuzo za Blogu nchini Kenya,  ni mradi wa  Umoja wa Wanablogu wa Kenya (BAKE) , wanakusudia kuwazawadia wnaablogu wanaobandika posti zao mara kwa mara, wenye maudhui sahihi na yenye kusaidia, wabunifu na wenye mambo mapya. Makundi mengine ni pamoja na: 

  • Blogu bora ya Teknojia
  • Blogu bora ya Picha
  • Blogu bora ya Uandishi wa Kiubunifu
  • Blogu bora ya Biashara
  • Blogu bora ya Chakula
  • Blogu bora ya Kilimo/Mazingira
  • Blogu bora ya Mitindo/Urembo/Nywele
  • Blogu bora ya Siasa
  • Blogu bora Mpya
  • Blogu bora ya Shirika
  • Blogu bora ya Mada
  • Blogu bora ya Michezo
  • Blogu bora ya Burudani/Mtindo wa Maisha
  • Blogu bora ya Kusafiri/li>
  • Blogu bora ya Mwaka nchini Kenya

Hapa chini kuna video ya kuzinduliwa kwa Tuzo za Blogu Nchini Kenya:

Blogu zinaweza kupendekezwa kwa kutumia kiungo hiki.  


Pigia kura Blogu ya Kenya Uipendayo

$
0
0

Zoezi la upigaji kura limeanza kwa ajili ya Tuzo za Blogu nchini Kenya kwa mwaka 2014:

Chama cha wanablogu wa Kenya (BAKE) hii leo [3 Machi 2013] kilizindua zoezi la kupendekeza majina ya wawaniaji wa tuzo hizo za wanablogu wa Kenya mwaka huu. Tuzo hizo hutolewa kwa wanablogu waandikao maudhui muhimu na yanayotolewa kwa ubunifu na muundo bunifu.

Wateuzi walichaguliwa na jopo la majaji lililohusisha wanablogu na waaandishi kutoka vyombo vya habari.

Kutolewa kwa orodha ya wateuzi huashiria kuanza kwa zoezi la kupiga kura kwa tuzo hizo.

Kupiga kura kutaanza kuanzia Machi 3, 2014 na kumalizika Aprili 30 2014

Unaweza kupigia kura blogu yako uipendayo kupitia tovuti ya www.blogawards.co.ke/vote

Mwongozo wa Kilimo cha Uyoga Nchini Kenya

$
0
0

Huu ni mwongozo hatua kwa hatua wa kilimo cha uyoga nchini Kenya:

Kutokana na mahitaji ya umma, sisi tulichukua mpango wa kuandaa mwongozo wa kusaidia wakulima wenye nia ya kuanzisha kilimo cha uyoga nchini Kenya

Mchakato wa kilimo cha uyoga waweza kugawanywa katika hatua kadhaa zifuatazo

1.Maandalizi ya mbolea

2.kutawanya mbegu/kupanda

3.kuweka kwenye makopo

4.ukuaji/matunda na kuvuna

Teknolojia ya Kiafrika: Mradi wa TechAfrique Watathmini Hatua Iliyofikiwa

$
0
0

 Le continent africain apparaît comme la nouvelle frontière mondiale du développement numérique. Ce développement provoque une nouvelle impulsion entrepreneuriale en Afrique, et notamment en Afrique francophone. Mais ce potentiel reste très largement méconnu en Europe ainsi qu'en France. 

Bara la Afrika linaonekana kuwa kiongozi mpya wa dunia katika maendeleo ya kidijitali. Maendeleo haya yamesababisha kukua kwa ujasiria mali mpya barani Afrika, hususani kwenye nchi zizungumzao Kifaransa. Lakini uwezo huu unabaki kuwa siri isiyofahamika huko Ulaya na Ufaransa.

Kubadili hali hii, Samiri, mwandishi wa blogu ya  Startup BRICS [fr] ilijikita kwenye miradi mipya katika nchi zinazoendelea, aliandaa safari za kiuchunguzi zilizoitwa  Mradi wa TechAfrique ili kugundua na kuorodhesha miradi iliyopo na ile mipa, miradi ya Fablabs, na kwenye maeneo mengine yanayofanana na hayo katika ubunifu wa kiteknolojia katika nchi zizungumzao Kifaransa pamoja na Kenya.

Shule 2,715 Kuunganishwa na Mtandao wa Intaneti Nairobi

$
0
0

Shule 2,715 jijini Nairobi, Kenya hivi karibuni zitaunganishwa na mtandao wa intaneti wa bure:

Wanachi Group [kampuni] imefikia makubaliano ya kutekeleza mradi wa thamani ya Dola za Marekani milioni 3 (Takribani KSh milioni 270) na kaunti ya Nairobi, ili kuunganisha shule 2,715 jijini Nairobi na mtandao wa intaneti.

Mradi huo ulizinduliwa leo na ifikapo mwezi Juni mwaka huu (ndio, ndani ya miezi mitatu), shule 245 za mfano zinatarajiwa kuwa zimeunganishwa tayari. Baada ya hapo, mradi huo utatathiminiwa na awamu ya pili itaanza ndani ya miaka mitatu hadi mitano.

“Pamoja na mtandao wa bure wa intaneti, kampuni hiyo itaipatia kila shule vifaa vya kidijitali kwa ajili ya kuunganisha televisheni kwa ajili ya matumizi ya kupata maudhui ya elimu kwa njia ya sauti kwa faida ya wanafunzi. Watoto wa shule za awali watapata vifaa hivyo pia ikiwa ni pamoja na televisheni ndogo,” ilisema taarifa ya kampuni hiyo ya Wananchi.

Namna Huduma ya Kuhamisha Fedha kwa Njia ya Simu Ilivyobadili Maisha ya Wakenya

$
0
0
M-Pesa payment till at a restaurant in Kenya. Photo released under Creative Commons by Wikipedia user Raidarmax.

Mahali pa kufanyia malipo ya M-Pesa kwenye hoteli nchini Kenya. Oicha imetolewa chini ya leseni ya Creative Commons na mtumiaji wa Wikipedia Raidarmax.

Mwezi Machi 2014 yatakuwa ni maadhimisho ya miaka saba tangu M-Pesa, huduma ya kufanya miamala ya kifedha kwa njia ya simu na huduma ndogo za kibenki, ilipoanzishwa Kenya na kampuni ya simu za mkononi iitwayo Safaricom. M-Pesa inafanya kazi kama benki; watumiaji wa huduma hiyo huhifadhi fedha kwenye simu zao na kutoa fedha kupitia wakala au duka la Safaricom kwa kuonyesha kitambulisho na namba ya simu.

Safaricom ilikuwa kampuni ya kwanza nchini Kenya kutoa huduma ya miamala ya kibenki. Inabaki kuwa  kampuni iliyotawala biashara hiyo hata leo, wakati kukiwa na makapuni kama Airtel, Orange na Yu ambayo pia yanatoa huduma kama hiyo.  Katika kusherehekea miaka saba ya huduma hiyo, Safaricom iliwahamasisha wa-Kenya kwenye mtandao wa Twita kutumia alama habari ya #BeforeMPESA [Kabla ya MPESA] kueleza namna huduma hiyo ilivyobadili maisha.

Hapa unaweza kusoma maoni yaliyojitokeza mara nyingi:

1. M-Pesa imewapa Wakenya mbadala wa kutunza fedha zao kwa usalama:

Kabla ya Mpesa

Kabla ya Mpesa: Namna watu walivyokuwa wakitunza fedha zao kwa usalama

2. Kenyans can now pay for almost anything through M-Pesa, even church offerings [sadaka] and electricity bills:

Ninaweza kulipa sadaka kwa urahisi nikiwa sebuleni kwangu, bila kulazimika kwenye kanisani

Hivi ndivyo nilivyokuwa nilisafiri kwenda benki kulipa bili yangu ya umeme

Kufupisha masimulizi huduma hii imefanya maisha yangu kuwa rahisi tangu nijiunge na Mpesa

Ukitoka kuzunguka, ukaishiwa na mafuta….unatembea mwendo mfupi tu unalipa na Mpesa

Baada ya kupata chakula na rafiki yako wa kike na kisha unakumbuka uliacha pochi yako nyumbani

Malipo ya mahari ilikuwa kazi…baada ya Mpesa sasa ni rahisi

Baadhi ya watu walizimia kwenye mistari mirefu benki wakati wa kufungua shule kwa sababu ya kuchoka kusubiri

Namna nilivyokuwa nikisubiri kutumiwa hawala ya fedha kwa njia ya posta

Kabla ya Mpesa na baada ya miaka saba ya Mpesa

3. M-Pesa inaweza kupatikana kwa simu yoyote:

@kebiwot Miaka saba ya MPESA lakini simu zina miaka 20

Bado, si kila mmoja anaifurahia M-Pesa

Baadhi ya Wakenya walitumia maadhimisho hayo kuonyesha hasira zao kwa M-Pesa na kuwakosoa wale wanaoisifia huduma hiyo:

Na hadithi hizi za kusadikika za MPESA

Namna Safaricom wanavyokuita kuja kukumaliza….

Samuel Gikuru alikuwa na wasiwasi na nia ya Safaricom na hata akaituhumu kampuni hiyo kuiba wazo la Mkenya alibuni huduma hiyo:

Hivi ni mimi pekeyangu au na mwingine amegundua kuwa Safaricom inafanya kila inachoweza kwa makusudi mazima kuua Vipaji vya kiteknolojia vinavyoibukia Kenya? Kuna hadithi inasimulia namna Mkenya alivyoibiwa wazo lake lenye thamani ya dola bilioni moja ambalo leo ndio limekuwa M-Psa. Kijana huyo mwenye akili inasemekana aliwaendea wakubwa wa Safaricom na wakamkatalia kuwa wazo lake lisingetekelezeka na ajabu miezi kadhaa baadae wakazindua huduma hiyo. Hiyo ndiyo hadithi iliyo kwenye midomo ya Wakenya wote. Hata hivyo, kitabu kipya kinadai kuwa mwajiriwa mwandamizi wa Vodafone ndiye aliyebuni M-Pesa mwaka 2003. Wakenya ni kama hawafaidiki na ubunifu wa M-Pesa ambao ndio unaiweka Kenya kwenye ramani ya dunia kama kituo cha ubunifu.

….Ukiwa na MPESA, faragha yako hailindiw. Kwa kutumia hela kidogo mpaka hata shilingi 10, mtu yeyote anaweza kukutambu kama mmiliki wa lini ya simu, kama namba yako imesajiliwa kwa huduma hiyo, kirahisi tu. Kama vile haitoshi watekaji wanaweza kutumia husuma hii kudai fedha. Ili kuhakikisha kuwa hawakamatwi au kuingia mtegoni kirahisi, wanafungua akaunti kwa kutumia kitambulisho bandia ambacho kinaweza kutengenezwa kinyume cha sheria pale kwenye mtaa wa River road Nairobi. Safaricom haifanyi chochote kuhakiki usahihi wa namba za kitambulisho.

Hadithi ya Mapenzi Kibera

$
0
0

Hii ni hadithi ya kusisimua ya mapenzi kati ya Sam, anayetoka Kibera, makazi ya masikini kwenye jiji la Nairobi, Kenya, na Alissa, anayetoka Minnesota, Marekani:

Bila shaka, hii ni hadithi ya mapenzi isiyo na kifani mwaka huu!!! Alissa anatoka Minnesota, huko Sam alizaliwa na kulelewa Kibera. Ilikuwaje ‘njiwa hawa wa mapenzi’ wakakutana?

Alissa alikuwa amekuja Kenya, na kwa muda wa miezi kadhaa, alikuwa anafanya kazi na watu wanaoishi Kibera. Kwa miezi kadhaa, akitumia Matatu (usafiri wa umma) kurudi nyumbani, alimwona Sam, kijana mwenye kipaji, aliyekuwa na kibanda cha ‘vito’ vya kiafrika pembeni mwa barabara. Siku moja, Sam alipokuwa akila ndizi pembeni mwa duka lake, akamwona msichana mrembo mzungu amekaa kulia mwa Matatu. Alishangazwa na kile alichokiona na akaamua kutumia shilingi tano zilizokuwa zimebaki mfukoni kumnunulia ndizi pia. Kwa hivyo akamwomba dada aliyekuwa kibandani ampe ndizi nyingine, nia yake ikiwa kumpatia mrembo yule mzungu ndizi hiyo. Bahati haikuwa yake, kwa sababu alipokaribia dirisha la upande ambapo msichana alikuwa amekaa, matatu ikaondoka kwa kasi. Akaikimbilia, lakini tayari alikuwa amechelewa. Matatu iliondoka ikiwa imembeba msichana wa ndoto zake.

Tovuti 50 Zilizotembelewa Zaidi Nchini Kenya

$
0
0

Je, unajua ni tovuti gani maarufu zinazotembelewa zaidi nchini Kenya? Soka posti ya James Wamathai kwenye blogu yake kufahamu zaidi:

Mengi yamebadilika tangu mwezi Januari, wakati nilipotoa orodha ya tovuti maarufu zaidi nchini Kenya. Tovti ya Budget airline Jambo Jet ilizinduliwa, gazeti linalomilikiwa na kampuni ya NMG liitwalo Nairobi News lilizinduliwa na kufanikiwa, tovuti ya burudani ya izvipi nayo ilianzishwa na Sauti Sol ilitoa video ya wimbo wao mpya iliyoibua mjadala mkali, lakini ilijipatia umaarufu, ‘Nishike”.

Kwenye orodha ya tovuti maarufu, kuna mabadiliko kadhaa kama unavyoona hapa.

Kenyan Post imeipiku Ghafla kama blogu maarufu zaidi nchini Kenya
Jumia, KRA, Career Point Kenya, Helb na Techweez zimepanda chati.
Niaje, The Star, Orange na Michezo Afrika zimeshuka umaarufu.
Ben Kiruthi, KU, Kenya Today na Kopo Kopo zimeingia kwenye orodha ya 50 bora.


Namna Teknolojia Inavyosaidia Watu Kujifunza —na Hata Kuokoa—Lugha za Dunia

$
0
0

Makala haya yameandikwa na mwandishi mwalikwa Allyson Eamer, mwanazuoni katika kitivo cha stadi za jamii na lugha katika Taasisi ya Teknolojia ya Chuo Kikuu cha Ontario. Toleo la makala haya  lilichapishwa awali kwenye blogu ya Mradi wa Ethnos.

Moja wapo ya lugha zinazopotea kwenye sura ya dunia hufa kila baada ya siku 10 hadi 14. Katika jitihada za kuziokoa lugha hizi zisipotee, wasemaji, wanazuoni na wataalamu wa Teknolojia wanaungana kuchungua namna teknolojia za kidijitali zinavyoweza kutumiwa katika kuhuisha lugha. 

Lugha zimekuwa katika hatari ya kupotea kadri muda unavyokwenda na kadri wazungumzaji wake wanavyohamia kwenye lugha nyinginezo zinazoonekana kuwa na nguvu ya kisiasa na kiuchumi. Mara nyingi, mabadiliko hayo hutokea kwa sababu ya ajenda za kikoloni za kujitanua ambazo huwafanya wenyeji, tamaduni, na ardhi zikitekwa na wajenzi wa falme zao. 

Katika hali inayotia matumaini, baadhi ya wasomi hawafurahishwi na kile kinachoweza kuitwa “Ku-Darwinishwa kwa lugha”, au kubaki kwa lugha zenye nguvu na kupotea kwa zile zisizo na nguvu. Hoja yao kuu ni: Je, si rahisi ste tukizungumza lugha moja?

Sitafafanua namna kila lugha ilivyo na tofauti za kipekee kwenye mtazamo wa kidunia: namna msamiati wa lugha unavyoofunua tunu za watu wanaoizungumza, namna maarifa ya asili yanavyobebwa katika muundo wa lugha, na namna sanaa, kujieleza, historiam utamaduni, uchumi na utambulisho vinavyofungamanishwa na lugha. Badala yake ninaendelea kwa imani kwamba, kama nilivgo mimi, wewe ndugu msomaji unaamini kwamba kupotea kwa lugha ni janga na kwamba wenye lugha hizi za asili duniani kote wameshuhudia wakinyang'anywa vingi.

Miniature DNF Dictionary  by Tomasz Sienicki (CC-SA-3.0)

Kamusi ndogo ya mfumo wa DNFpicha na Tomasz Sienicki (CC-SA-3.0)

Teknolojia inaweza kuwaunganisha walimu na maudhui ya lugha na watu wanaotamani kujifunza lugha hizo duniani kote kwa wakati ule ule. Teknolojia inaweza kuhifadhi lugha zilizokwenye hatari ya kupotea kwa kutumia mfumo wa sauti. Inaweza kutengeneza na kusambaza mitaalama na zana za kujifunzia kirahisi na kwa wepesi. Inaweza kurahisisha kujifunza kwa kujitegemeea kupitia michezo, kupakua programu na viwezeshi vingine. Ianweza kuwaunganisha walimu na wanafunzi wa lugha kwa namna mbalimbali.

Watu wenye fikra za kuleta mabadiliko wanaunganisha nguvu za kiteknolojia kuzileta lugha kutoka kwenye hatari ya kupotea, na katika hali nadra sana, kuzifufua lugha zilikwisha kufa.

Hapa ni pitio fupi la namna mbalimbali ambazo teknolojia ya kidijitali zinavyotumiwa katika jitihada hizi:

Ulaya

Marekani Kaskazini

  • CD-ROM ya kozi ya kujifunza mwenyewe  imeundwa katika lugha ya Navajo, inayozungumzwa kusini magharibi mwa Marekani
  • Wanaojifunza Kicherokee, lugha inayozungumzwa Marekani Kusini Kati, wanaweza kuwasiliana bila kuonana.
  • Jamii ya Ojibwe huko Manitoba, Canada, wanatumia zana ya simu za iPhone kuhuisha lugha zao, kama wanavyofanya Wawinnebago wa Marekani ya Magharibi

Afrika

  • Maktaba zinaundwa kwa ajili ya lugha zinazozungumzwa tu nchini Kenya.
  • Hadithi za kale zinarekodiwa katika lugha za asili nchini Mali.
  • Kampuni ya kujifunza lugha mtandaoni inatoa kozi ya lugha za miluzi kwenye visiwa vya Canary nchini Uhispania.

Marekani ya Kati na Kusini

Asia

Ncha ya Kaskazini

  • Mfululizo wa masomo ya mtandaoni  yanapatikana katika lugha ya Inuktitut, moja ya lugha ya nchi za ncha ya kazkazini mwa dunia.

Mashariki ya Kati

  • Masimulizi ya mtandaoni katika lugha ya Chaldean, inayozungumzwa nchini Irak, inaweza kuwasaidia wazungumzaji kujifunza kwa usahihi lugha hiyo.

Nchi za Bahari ya Pasifiki

Kwa habari za karibuni zaidi kuhusu teknolojia kuhusu matumizi ya elimu ya lugha za asili, angalia kwenye tovuti ya hifadhi ya maudhui ya Allyson Eamer

Viewing all 29 articles
Browse latest View live